SUPU YA KABICHI NA KUKU Unapopenda chakula Fulani mara nyingi unatafuta namna mbalimbali ya kukipika na kukiandaa ili uweze kukila na kukifurahia mara kwa mara.
Mimi napenda sana kabichi,ni mboga ambayo siwezi kuichoka,naipika katika namna mbalimbali ilimradi tu niweze kuila.Mara nyingi najikuta nakula kabichi katika milo yangu yote ya siku.
Supu ya kabichi na kuku ni kifungua kinywa ninachokipenda sana,na hivi ndivyo ninavyoandaa supu:
Mahitaji
1.Kuku
*.Kuku ½ kilo (au mapaja matano)
*.Vitunguu saumu ½ kijiko cha chai
*.Pilipili manga ½ kijiko cha chai
*.Maji ya tangawizi ½ kijiko cha chai (sugua tangawizi kisha kamua maji yake)
*.Vinegar kijiko 1 cha chakula (unaweza tumia ndimu au limao)
*.Chumvi kwa ladha uipendayo
2.Mboga
*.Kabichi vikombe 2
*.Karoti ½ kikombe
*.Hiho ½ kikombe
*.Vitunguu maji ½ kikombe
*.Kata mboga vipande vikubwa
Njia
1.katika sufuria weka viungo vyote vya namba moja,changanya vizuri kisha chemsha adi nyama ichuche maji.Ongeza maji kiasi,usawa wa nyama ilipoishia.Ongeza mboga zote kwa pamoja ,funika na chemsha kwa moto mdogo sana.Mboga zikisinyaa tu,zima jiko.supu tayari kwa kunywa
*.Ni muhim kupika kwa moto mdogo ili mboga zisipoteze vitamin C na zisiive sana
*.Hakikisha mboga haziivi sana,zinatakiwa kupata joto kidogo tu ili kuondoa ubichi na zilainike.
*.Uzito wa supu utatokana na kiasi cha maji uliyoongeza,ukitaka iwe nyepesi basi wakati wa kuongeza maji,ongeza mengi zaidi .Usiongeze maji kwenye supu baada ya kuweka mboga,yataharibu kabisa utamu wa supu.Maji yote weka kwenye kuku kabla hujaongeza mboga.
Supu hii unaweza kunywa wakati wowote.Unaweza kuisindikiza kwa aina yoyote ya mkate au biskuti za chuvi ambazo ni maalum kwa kunywea supu.Kama uko kwenye diet au ni mtu unaejali kula yako basi brown bread inafaa zaidi.
Hapa jikoni natumia sana supu hii kama kifungua kinywa.
ONJA MABADILIKO,KULA KILICHOBORA ZAID
No comments:
Post a Comment