KANUNI ZA KUPUMZIKA KUZAA
1.Kanuni ya kutogusanaKuacha tendo la ndoa kabisa wakati wa siku zote za uzazi, yaani:
*.bwana asimwage mbegu nje
*.wala mapajani
*.wala kinenani
*.wala kugusana viungo vya uzazi nje, kwa sababu tone dogo la shahawa linaweza kutoka kabla ya mshushio au mshindo na mbegu zinaweza kuingia katika ute wa uzazi uliopo nje na kuogelea katika mifereji ya ute wa uzazi mpaka ukeni na kusababisha mimba.
*.wala kutumia dawa za majira
*.wala kutumia kondomu siku za uzazi.
1.Kanuni za mapema
a.kuacha tendo la ndoa wakati wa hedhi.
b.kuacha tendo la ndoa wakati wa damu kidogo na siku 3 baadaye.
c.kuacha tendo la ndoa wakati wa ute wa uzazi na siku 3 badaye.
d.kufanya tendo la ndoa wakati wa siku zisizo na uzazi, ukavu, ute mzito usiobadilika, aina ya majimaji yasiyobadilika jioni tu, si kesho yake.
?Jioni tu: kwa sababu mama ana hakika kama ana ute wa uzazi au siyo.
?Si kesho yake: Mama hawezi kutofautisha kama ute ni wa
mume tu au kama mwenyewe ameanza pia
kupata ute wa uzazi.
1. Kanuni ya kileleKuacha tendo la ndoa siku ya kilele na siku tatu baada ya kilele. Kuanzia siku ya nne baada ya kilele tendo la ndoa linawezekana siku na saa yoyote mpaka mwisho wa mwandamo.
No comments:
Post a Comment