Saturday 26 October 2013

Mahusiano

Single Ladies...
Mchumba siyo mume. Mume anawajibika kisheria na kibiblia kumtunza mke wake na watoto lakini mchumba hawajibiki kukutunza. Unapopata mchumba anayekusaidia kifedha umshukuru sana na usimchukulie kuwa ni wajibu wake. Haifai wala haipendezi kuwa unamuomba hela mchumba wako kila wakati. Ndio mnapendana sana, lakini nikuambie kitu mwanaume akiona kila siku binti unamlilia shida za hela na hamjaoana ataazimia kukuacha kimya kimya. Sio kwamba hapendi kukusaidia, ila ataona kwamba wewe unampenda sababu anakusaidia. Hakuna asiye na shida na hela, shida tumeumbiwa wanadamu..

No comments:

Post a Comment