Thursday 28 November 2013

Misemo

MISEMO NA MAFUNZO YAKE!!!
1. Hata kama mtu ni mwerevu, huwezi kuwadanganya watu wote kwa muda mrefu. Siku moja utagunduliwa, kwa sababu "siku za mwizi ni arobaini" au "habari za uwongo zina ncha saba.
2. Ili binadamu aishi na kufaulu katika maisha yake, hana budi kujitolea na kupambana na hali yoyote katika mazingira.
3. Kuwa na tamaa inaweza kuua. Kama wahenga walivyosema:- Njia mbili zilimshinda Fisi.
4. Ujinga na woga husababisha taabu na hasara kubwa ulimwenguni
5. usimdharau adui ijapokuwa ni dhaifu. Ni kwamba akufaaye kwa dhiki ndiye rafiki.
6. Mtu akifanya kazi kwa bidii hufanikiwa. Au maskini hachoki, akichoka keshapata.
7.Asiyesikia la mkuu huvunjika guu. Hii ni kwamba hatuna budi kuwatii wazazi wetu tukitaka kuuelewa ulimwengu.
8. Si utu kwende kwa uliyempa zawadi na kumwambia akurudishi zawadi yako
9. wivu hangamiza familia nyingi ulimwenguli
Namba kumi naomba wewe uzaja. Ni kwamba kama nawe una msemo na basi karibu jumuika nami....

No comments:

Post a Comment