Friday 29 November 2013

Habari

Njia mpya ya Reli Afrika Mashariki
28 Novemba 2013 16:32
Kenya imezindua rasmi ujenzi wa njia ya Reli
itakayounganisha kanda ya Afrika Mashariki
na eneo la maziwa makuu ujenzi
utakaofadhiliwa na serikali ya China.
Reli hiyo itaunganisha Kenya na Sudan
Kusini, DR Congo na Burundi.
Sehemu ya kwanza ya njia hiyo ya reli ,
itaunganisha bandari ya Mombasa na Mji
mkuu Nairobi na kupunguza muda wa
safari kati ya miji hiyo kutoka masaa 15 hadi
masaa manne tu.
Huu bila shaka ndio utakuwa mradi
mkubwa Zaidi kuwahi kujengwa tangu nchi
hiyo kujipatia uhuru miaka 50 iliyopita.
Mradi huo utagharimu dola bilioni 5.2 kiasi
kikubwa cha pesa hizo kikitolewa na
Uchina.
Baadhi ya wakenya wanalalamika kuwa
tenda hiyo imetolewa kwa kampuni ya
kichina kwa njia isiyofaa.
Rais Uhuru Kenyatta katika hafla ya uzinduzi
huo amesema kuwa mradi huu ndio
utakuwa kumbukumbu kubwa ya utawala
wake Kenya.
Mkataba wa ujenzi wa njia hiyo ya reli,
ulifikiwa kati ya Rais Kenyatta na mwenzake
wa China Xi Jinping mnamo mwezi Agosti
mjini Beijing.
Pia kuna matumaini kuwa njia hiyo ya reli
itapunguza msongamano mjini Mombasa
moja ya bandari yenye shughuli chungu
nzima barani Afrika.
Njia ya reli iliyoko sasa, ni ile iliyojengwa
enzi za ukoloni.
Baada ya kukamilika kwa sehemu ya
kwanza ya reli hiyo mjini Nairobi, mwaka
2017, itaendelezwa hadi Magharibi mwa
DRC hususan mjini Kisangani, Rwanda,
Burundi na Sudan Kusini.
"Tunachokifanya hapa leo, kitaleta mageuzi
makubwa sio nchini Kenya tu bali katika
kanda nzima ya Afrika Mashariki,’’ alisema
Rais Kenyatta akitaja mradi huo kama jambo
la kihistoria.
Aliongeza kusema kuwa mradi huu ni moja
ya miradi mikubwa katika maono yake ya
maendeleo itimiapo mwaka 2030
kuboresha hali ya miundo msingi nchini
humo.

No comments:

Post a Comment