Tuesday 10 December 2013

Siri ya Mbunge kushinda uchaguzi ni ahadi
zake kutatua shida za Wananchi,na ili aweze
kushinda uchaguzi tena akigombea,ni lazima
awe karibu na wananchi ili kujua shida zao
na kuzitatua...
Siri ya Penzi bora ni wewe kuwa karibu na
Mpenzi wako maana huyo ndio jimbo lako la
Uchaguzi,Jua ana shida gani,ana yapi
yanamsibu,Hisiazake ziko sawa??Na kumpa
furaha....
Ukichaguliwa kuwa Mbunge halafu hujui
Jimboni kwako nini kinaendelea usitegemee
utashinda Uchaguzi Ujao,utakuta wananchi
wamekuchoka na wapinzani wako
watakuwawametumia udhaifu wako wa
kutojua jimbo lako linataka nini kupenyeza
sumu wapewe wao jimbo...
Ukijifanya Uko bize kwa mpenzi wako,oh
kazinyingi,mara ohh nna excel sheet
zinanisumbua mara vile,utachokwa,na
ukichokwa watu wanampa Kura mtu
mwingine
Mheshimu Mpenzi wako kama Mbunge
Mjanjaanavyoheshimu Jimbo lake la
uchaguzi,ukijifanya Bize usishangae kukuta
Jimbo limechukuliwa wewe huna habari...
Kama uko Bize, Dont Fall in Love,Penzi ni Ajira
kama ajira zingine na linahitaji Muda na
Concentration,usilichukulie Poa maana na
lenyewe litakuchukulia Poa.
je,Unajua kinachojiri Jimboni kwako sasa
hivi??Au una-assume jimbo liko salama
wakati viwavi-jeshi na tunutu wameshacover
nafasi??WATCH OUT...JALI JIMBO LAKO

No comments:

Post a Comment