Monday 28 October 2013

Afya

MLANGO WA TUMBO LA UZAZI, VIKUNJO VYAKE NA AINA YA UTE
A. Katika mlango wa tumbo kuna vikunjo mbalimbali-
*.vikunjo vya L, S, na P vinatengeneza ute wa uzazi Estrogen ikizidi.
*.vikunjo vya G vinatengeneza ute usio na uzazi Progesteron ikizidi
1.Ute wa G kazi yake ni:-Kufunga mlango wa tumbo la uzazi. Mbegu za baba na vijidudu vya magonjwa haviwezi kupita. Ute wa G hauna uzazi.
1.Ute wa L kazi yake ni:-
*.Kuchuja mbegu dhaifu 400,000,000→200.
*.Kufungia mbegu zenye nguvu katika vikunjo vya S. Ute wa L una uzazi.
1.Ute wa S kazi yake ni:-
*.Kulisha mbegu za baba, zinaishi siku 3-5. Katika mazingira yasiyo na uzazi zinakufa kabla ya nusu saa.
*.Ute wa S unaziwezesha mbegu kuingia katika tumbo la uzazi.Ute wa S una uzazi.
1.Ute wa P kazi yake ni:-
*.Kuyeyusha ute wa G na kufungua mlango wa tumbo la uzazi.
*.Pamoja na Enzyms wa Z-granula, huyeyusha ute wa L na kufungua vikunjo vya S ili mbegu ziweze kutoka na kuingia katika tumbo la uzazi na kufuata kijiyai.
*.Huzisukuma mbegu ndani.
*.Kuchuja mbegu za baba.Ute wa P una uzazi.
1.Ute wa F kazi yake:- Haijulikani.
MIANDAMO
1.AINISHO:Mwandamo ni muda kutoka siku ya kwanza ya hedhi mpaka
siku ya kwanza ya hedhi inayofuata .
2. Mabadiliko mbalimbali katika mwandamo: damu, ukavu, ute mzito,
ute wa kuteleza, ukavu tena n.k
3. Aina ya miandamo.
(1) Mwandamo wa wastani, siku 25-34
(2) Mwandamo mfupi, siku 18-24
(3) Mwandamo mrefu, siku 35-50 au zaidi
(4) Mwandamo bila utaratibu.
*Hakuna sababu ya kurekebisha mwandamo, ni maumbile yake.
Wasitumie dawa ya chachu bandia, zina madhara mengi, pia zinaleta utasa.
SIKU YA KIJIYAI KUCHOPOKA
Umuhimu wa kilele ni kwamba kijiyai kinachopoka hapa, yaani siku ya kilele yenyewe, au siku moja baada ya kilele, au siku ya pili baada ya kilele.
*Kama kawaida kijiyai kimoja tu kinachopoka katika mwandamo mmoja. Lakini inaweza kutokea kwamba vijiyai viwili au vitatu vinachopoka. Lakini vyote vinachopoka siku moja tu, yaani katika masaa 24. Vijiyai vyote vinaishi masaa 24 tu. Hakuna kijiyai kinachoiva tena mpaka mwandamo unaofuata.
DALILI ZA KUCHOPOKA KIJIYAI
1.Kilele.
2.Mdomo wa uke unavimba upande kijiyai kinapoiva.
3.Tezi kwenye nyonga inavimba upande kijiyai kinapoiva

No comments:

Post a Comment