JIFUNZE KUPIKA SAMAKI KATIKA OVEN KWA KUTUMIA FOIL
NI RAHISI, NAFUU NA HARAKA SANA KUANDAA AINA HII YA MAPISHI YA SAMAKI KWA KUTUMIA FOIL NA KUOKA KATIKA OVEN LAKINI SAMAKI ATATOKA KAMA AMECHEMSHWA NA AKIWA NA LADHA SAFI SANA BILA YA KUPOTEZA VIRUTUBISHO VYOTE MUHIMU.
MAHITAJI
1pc kitunguu maji kikubwa
1 pc limao kubwa
5 gram binzali
5 gram chumvi
5 gram pili pili manga
1 pc pili pili hoho kubwa
50 gram tomato pest ( nyanya ya kopo)
kipande cha foil kutokana na ukubwa wa samaki
JINSI YA KUANDAA FATILIA muonekano wa samaki akiwa mbichi tayari umeshamsafisha vizuri kwa maji baridi na mapishi haya unaweza tumia kwa samaki aina ya sato, sangara, kibua, change, jodari au kole kole na akaiva na ladha safi kabisa. mchanganyiko wa vitunguu, pilipili hoho, maji ya limao, binzali, chumvi, pili pili manga na nyanya ya kopo, baada ya kuchanganya pamoja kasha mpakae samaki pande zote mbili ulizompasua ili mchanganyiko huu uingie vizuri katika nyama kasha mabaki ya huo mchanganyiko mjazie tumboni kisha mfunike vizuri na foil muweke katika oven tayari ikiwa na moto.
Jana mchana niliporudi nyumbani niliandalia samaki aina ya sato pamoja na maharage ya Nazi na ugali wa mahindi.
Unaweza kumpika katika oven kwa dakika 30 kwenye moto wa degree 200 hadi 250 pia kwa mtindo huu unaweza kumchoma katika jiko la mkaa akiwa hivi hivi katika foil na akaiva safi kabisa
Baada ya nusu saa samaki wako atakua ameiva na atakua na muonekano mzuri na ladha safi sana tayari kwa kuliwa
No comments:
Post a Comment