Friday 15 November 2013

Mahusiano

Kuna watu ili muonane na wapenzi wenu lazima muwe na shughuli maalum,wengine hata muwe na shughuli bado mpenzi hatokei..Ila yeye akikuhitaji ili aje kucheza SKELEWU kwenye mwili wako hutakiwi kuwa na excuse na ikitokea unayo basi ugomvi utakaozuka hapo hauamuliwi na NATO wala Koffi Annan
Eti na wewe Ur in a Relationship na umeanza kuulizia Bei ya Mashela ya Harusi..POLE!
Kuna Tofauti ya Kudate na Mwanaume na Kudate na Ambulance ya Mwananyamala Hospital. Ni ambulance tu huitwa kwa shughuli maalum na zikishamaliza kupeleka mgonjwa basi umuhimu wake umeisha
Kufanywa Mjinga Mara moja TULIKUELEWA,lakini kuendelea kufanywa Mjinga kwa Miaka Mitatu tuna wasiwasi mwenzetu wewe ni MSUKULE…Japokuwa inauma kumpoteza mtu unayempenda lakini ili Serikali ya Moyo wako ibaki salama unapaswa kufanya maamuzi magumu
Akikutumia Meseji kuomba Ngololo mwambie kabisa, I AM NOT UR AMBULANCE….Kaziyako ni kubeba Mgonjwa tu,akipona unaachwa Parking bila kazi mpaka apatikane mwenye Kifafa uitwe tena..
Dear Ambulance,PLEASE WAKE UP
by Seth De Jesus Giovani

No comments:

Post a Comment