JIFUNZE KUTENGENEZA YAI JICHO LA NG'OMBE NA KIPANDE CHA MKATE
RECIPE SAFI KABISA YA KUTENGENEZA KITAFUNWA HIKI KWA WAKATI WA MAPUMZIKO HAYA MAREFU.
MAHITAJI
1 Yai
1 kipande cha mkate
1/2 kijiko kidogo cha chai siagi
5 gram chumvi
2 gram pili pili manga Chukua kipande cha mkate kunja nusu kisha kata mduara kati kati Huu ndio muonekano wa mduara baada ya kukata
Chukua brush na kisha paka pande zote mbili siagi.
Chukua kipande cha mkate kisha weka katika kikaango chenye moto wa wastani ili isiungue.
Kisha pasua yai na mimina kati kati ya mkate
Kisha nyunyizia chumvi na pili pili manga kwa juu ya yai nali mkate.
Baada ya dakika 3 hadi 4, upande mmoja uta.kua umeiva geuza upande wa pili
Upande wa pili pika kwa dakika 2 tu utakua umeiva pia
No comments:
Post a Comment