Sunday 3 November 2013

Afya

Hapa chini ni baadhi tu ya vipimo muhimu kwa wanandoa watarajiwa kupima
1. Kupima kundi la damu na Rh factor;kuna makundi ya aina nne(4) ya damu ambayo ni
A, B, AB na O. Makundi yote haya yanaweza yaka ni positive(+) au Negative(-) ambayo
ndio tunaita Rhesus factor kwa kifupi Rh. Hivyo tukinyumbulishatutapata makundi kwa mtindo
huu: A+, A-, B+, B-, AB+, AB-, O+ na O-. Sasa, hali ya kua na positive(+) au negative(-)
hakuathi afya yako. Tatizo linakuja wakati mama/dada akiwa ana kundi la damu lenye
Rh-(negative) na mwanaume/kaka akiwa na kundi la damu lenye Rh+(positive). Wanapokutana
watu hawa kimwili wanaweza kupata mtoto ambaye ana kundi la damu lenye Rh+(positive).
Kuna wakati kwa bahati mbaya damu ya mtoto inagusana na ya mama anapokua tumboni au anapozaliwa.
Hii itasababisha reaction ya kukutana damu ambayo ina Rh+ kutoka kwa mama na damu ambayo ni
Rh- ya mtoto na hivyo kusababisha hali mbaya kwa mtoto kama matatizo ya ubongo, upungufu wa
damu na hata kifo cha mtoto.
Kitu kizuri ni kwamba hali hii huweza kuzuilika endapo itajulikana mapema. Kuna dawa ya sindano
inaitwa Rhogam na kitaalamu zaidi inaitwa Rh immunoglobulin (RhIg) ambayo hupunguza reaction
ya zile damu zisizopatana baada ya kukutana. Inashauriwa kwa mama ambaye ana hali hii achomwe sindano hii katika weki ya 28 ya umri wa mimba yake. Kwa dozi moja ya Rhogam huisha nguvu yake katika wiki ya kumi na mbili (12), hivyo mama huyu atapewa dozi nyingine ya Rhogam ndani ya masaa 72 baada ya kujifungua kama mtoto ni Rh+. sindano hii pia inaweza kutolewa kwa
mwanamke mwenye hali hii wakati mimba imeharibika au kwa aliye toa mimba.

No comments:

Post a Comment