Friday 15 November 2013

Utamaduni

Utamaduni, mila na desturi

Hali ya mvuto wa mfumo ya jamii wa Tanzania ni kivutio kikubwa kwa masuala ya utamaduni, uchumi na utalii.Hadithi za watu wa kale, ngoma za asilia na aina ya ngoma zinatofautiana kati ya kabila na kabila.Wanapocheza, Wamakonde kuchezesha viuno vyao kwenda sambamba na ngoma ya “sindimba”, Wazaramo humezwa na maandamano ya “mdundiko”.Wamaasai huruka kwa mpangilio maalum huko wakitoasauti nzito ambazo zinaweza kumwogofya simba dume!Matumizi ya nyoka hai na kucheza na nyoka wakubwa kama chatu kunakofanywa na Wasukuma wakati wanacheza ngoma ya “Bugobogobo” hakuwezi kusahaulika kwa mgeni.Kila kabila kati yamakabila 120 ya Tanzania ina ngoma yake na staili zake za uchezaji ambazo zinapumbaza kwa kukazia macho zinafurahisha na kuvutia kijinsia.
Aina mbalimbali ya mavazi pia hutoa mvutowa aina yake kwa mgeni.Wanaume wa Kimasai huvaa vazi ambalo halifuniki mwili wote huku wakitembea na mikuki, virungu na visu vikubwa.Kwa upande wao, wanawake wa Kimasai hujaza tele shingo zao, mikono, miguu na masikio yao na vitu vya thamani vikiwemo shanga na hadi aina nyingine za madini.Wanaume wa Kimasai hupakaza miili yao na udongo mwekundu uliochanganywa na mafuta yatokanayo na wanyama na husuka nywele zao.
Wamakonde nao huchonga meno yao na kuchanja nyuso na miili yao taaluma inayotamanisha.Wamakonde ni wataalam wa kuchonga vinyago vinavyoonyesha matatizo ya binadamu, mapambano, mapenzi, tamaa, wema, ubaya na mshikamano vitu ambavyo vinavutia sana na kuamsha fikra.
Wakazi wa pwani na visiwani hupamba mikono, miguu, midomo na kucha kufuatana na tukio shughuli ambayo huleta mvuto mkubwa.
Kati ya makabila ya namna ya pekee ni makundi ambayo yanakadiria kutoweka yaishiyo kati ya Tanzania.Makabilahaya ni ya Wasandawe (wanahusiana na Waethopia) ambao jirani zao ni wa Iraqw gorowa na burungi na Wadzapi ambao pia hujulikana kama Watindiga na Wakangeju na Wahontetot - wanaohusiana na kabila la Khosa la Afrika Kusini ambao huzungumza lugha za “click”.Wandorobo pia wanazungumza lugha hiyo lakini wameiga zaidi utamaduni wa nje ya mazingira yao.Watanzania hao ni wa kuhamahama, wachumaji matunda, wawindaji wakusanyaji chakula, na wavuvi waishio katika eneo linalozunguka Ziwa Eyasi ambalo liko kilomita chache kutoka bonde maarufu la Ngorongoro.Inasemekana kwamba idadi ya watu hawa kwa sasa haifikii 500 wakati mwaka 1965 walikuwa zaidi ya 30,000.
Wito hapa ni kuisaidia Serikali ya Tanzania kuwaokoa watu hao wasifikie ukingo wa kutoweka.Kwa maana hiyo, maeneo yanayozunguka Ziwa Eyasi ni bora kabisa ya kufanyia utafiti wa kisayansi wa elimu ihusuyo habari za asili na maendeleo yabinadamu kwa ajili ya kumbukumbu za baadaye.Kinachojitokeza ni kwamba ni vyema kutambua kuwa huu ni wakati muafaka wa kufanya uchunguzi ama vile watu hao watakuwa wametoweka kabisa.

No comments:

Post a Comment